sw_tn/luk/01/76.md

831 B

ndiyo, na wewe

Zakaria anatumia kauli hii kuanza hotuba yake moja kwa moja kwa mtoto wake. Unaweza kuwa na njia ile ile ya kuhutubia moja kwa moja katika lugha yako.

huyu, mtoto, ataitwa nabii

Watu watatambua kwamba huyu ni nabii. Hii inaweza ikasemwa katika mtindo wa kutendea. NI: "watu watajua kwamba wewe ni nabii."

wa aliye Juu Sana

"ambaye anamtumikia aliye Juu Sana." Hii inarejea kwa Mungu. NI: "ambaye anazungumza kwaajili ya Mungu aliye Juu Sana."

kwenda mbele za uso wa Bwana

Nahau hii inamaana "kwenda mbele za Bwana" au "kuja mbele za Bwana."

kuwapa maarifa ya wokovu watu wake

"kuelezea wokovu kwa watu wake" au "hivyo watu wake waweze kufahamu wokovu"

kwa msamaha wa dhambi zao

"kupitia msamaha wa dhambi zao." Pia inaweza kusemwa katika mtindo wa kutendea. NI: "kwa sababu Mungu amewasamehe"