# ndiyo, na wewe Zakaria anatumia kauli hii kuanza hotuba yake moja kwa moja kwa mtoto wake. Unaweza kuwa na njia ile ile ya kuhutubia moja kwa moja katika lugha yako. # huyu, mtoto, ataitwa nabii Watu watatambua kwamba huyu ni nabii. Hii inaweza ikasemwa katika mtindo wa kutendea. NI: "watu watajua kwamba wewe ni nabii." # wa aliye Juu Sana "ambaye anamtumikia aliye Juu Sana." Hii inarejea kwa Mungu. NI: "ambaye anazungumza kwaajili ya Mungu aliye Juu Sana." # kwenda mbele za uso wa Bwana Nahau hii inamaana "kwenda mbele za Bwana" au "kuja mbele za Bwana." # kuwapa maarifa ya wokovu watu wake "kuelezea wokovu kwa watu wake" au "hivyo watu wake waweze kufahamu wokovu" # kwa msamaha wa dhambi zao "kupitia msamaha wa dhambi zao." Pia inaweza kusemwa katika mtindo wa kutendea. NI: "kwa sababu Mungu amewasamehe"