sw_tn/lev/10/05.md

827 B

Hivyo wakakaribia

"Kwa hiyo Mishaeli na Elzafani wakakaribia"

kuwachukua wangali wamevaa kanzu zao za kikuhani

Waliibeba miili ya Nadabu na Abihu, ambayo ilikuwa ingali kwenye kanzu za kikuhani

Eliezari...Ithamari

Haya ni majina ya wana wa Aroni.

Msiache wazi nywele za vichwa vyenu, wala msirarue nguo zenu,

Yahweh anawaambia Aroni na wanawe wasionyeshe ishara yoyote ya nje ya huzuni au kuomboleza.

ili kwamba msije mkafa

"ili kwamba msife"

asilikasirikie kusanyiko zima

"Kusanyiko" hapa humaanisha kutaniko zima la Israeli, siyo kikundi cha viongozi tu. : "asiwakasirikie watu wote wa Israeli"

nyumba yote ya Israeli

"Nyumba" hapa huwakilisha watu wa Israeli. "watu wote wa Israeli"

kwa ajili ya hao ambao Yahweh amewaangamiza kwa moto

"kwa ajili ya wale ambao Yahweh aliwaua kwa moto wake"