sw_tn/heb/02/07.md

24 lines
1.1 KiB
Markdown

# mdogo kuliko malaika
Mwandishi anamuongelea mwanadamu kuwa sio wa muhimu kuliko malaika kana kwamba wanadamuwamesimama katika nafasi amabayo ni ya chini kuliko nafasi ya malaika. AT: "mdogo kuliko malaika."
# amemfanya mtu...amevika... miguu yake... kwake
Maneno haya sio kwa ajili ya mlengwa mmoja bali inajumuisha wanadamu wote, inajumuisha wanaume na wanawake.AT: "amewafanya wanadamu... amewavika...miguu yao... kwao"
# umemvika utukufu na heshima
zawadi ya utukufu na heshima zinaongelewa kana kwamba ni shada la majani lililowekwa kichwani mwa mshindi wa mchezo. AT:"umewapa utukufu mwing na heshima"
# Umeweka kila kitu kiwe chini ya miguu yake
Mwandishi anamuongelea mwanadamu kuwa na utawala juu ya kila kitu kana kwamba wamesimama juu ya kila kitu. AT: "Umewapa kumiliki juu ya vitu vyote"
# Hakuacha kitu chochote kisicho kuwa chini yake
maneno mawili hasi yanamaanisha kwamba vitu vyote vitawekwa chini ya Kristo. AT: "Mungu alifanya kila kitu kuwa chini yao"
# Hatuoni vitu vyote vikiwa chini yake
tunafahamu kuwa bado wanadamu hawajawa wamiliki wa kila kitu