# mdogo kuliko malaika Mwandishi anamuongelea mwanadamu kuwa sio wa muhimu kuliko malaika kana kwamba wanadamuwamesimama katika nafasi amabayo ni ya chini kuliko nafasi ya malaika. AT: "mdogo kuliko malaika." # amemfanya mtu...amevika... miguu yake... kwake Maneno haya sio kwa ajili ya mlengwa mmoja bali inajumuisha wanadamu wote, inajumuisha wanaume na wanawake.AT: "amewafanya wanadamu... amewavika...miguu yao... kwao" # umemvika utukufu na heshima zawadi ya utukufu na heshima zinaongelewa kana kwamba ni shada la majani lililowekwa kichwani mwa mshindi wa mchezo. AT:"umewapa utukufu mwing na heshima" # Umeweka kila kitu kiwe chini ya miguu yake Mwandishi anamuongelea mwanadamu kuwa na utawala juu ya kila kitu kana kwamba wamesimama juu ya kila kitu. AT: "Umewapa kumiliki juu ya vitu vyote" # Hakuacha kitu chochote kisicho kuwa chini yake maneno mawili hasi yanamaanisha kwamba vitu vyote vitawekwa chini ya Kristo. AT: "Mungu alifanya kila kitu kuwa chini yao" # Hatuoni vitu vyote vikiwa chini yake tunafahamu kuwa bado wanadamu hawajawa wamiliki wa kila kitu