sw_tn/gen/18/01.md

28 lines
615 B
Markdown

# Mamre
Hili lilikuwa jina la mwanamume aliyemiliki mialoni.
# mlangoni pa hema
"katika uwazi wa hema" au "katika kuingilia kwa hema"
# joto la mchana
"wakati wa jua kali la mchana"
# Akatazama juu na, tazama, akaona wanaume watatu wamesimama.
"Alitazama juu na kuona, tazama, wanamume watatu walikuwa wamesimama"
# tazama
"ghafla". Neno "tazama" hapa linatuonyesha kitakachofuata ni cha kushangaza kwa Abrahamu.
# mbele yake
"karibu" au "pale". Walikuwa karibu na yeye, lakini umbali wa kutosha kwa yeye kuwakimbilia.
# kuinama
Hii ina maana kuinama chini na kuonyesha unyenyekevu na heshima kwa mtu.