# Mamre Hili lilikuwa jina la mwanamume aliyemiliki mialoni. # mlangoni pa hema "katika uwazi wa hema" au "katika kuingilia kwa hema" # joto la mchana "wakati wa jua kali la mchana" # Akatazama juu na, tazama, akaona wanaume watatu wamesimama. "Alitazama juu na kuona, tazama, wanamume watatu walikuwa wamesimama" # tazama "ghafla". Neno "tazama" hapa linatuonyesha kitakachofuata ni cha kushangaza kwa Abrahamu. # mbele yake "karibu" au "pale". Walikuwa karibu na yeye, lakini umbali wa kutosha kwa yeye kuwakimbilia. # kuinama Hii ina maana kuinama chini na kuonyesha unyenyekevu na heshima kwa mtu.