sw_tn/gen/12/01.md

32 lines
947 B
Markdown

# Sasa
Neno hili linatumika kuweka alama sehemu mpya ya simulizi.
# Nenda utoke katika nchi yako, na toka kwa ndugu zako
"Nenda kutoka nchini kwako, kutoka katika familia yako"
# Nitakufanya uwe taifa kubwa
Hapa "nitakufanya" ni umoja na ina maana ya Abramu, lakini Abramu anawakilisha vizazi vyake. "Nitaanzisha taifa kubwa kupitia kwako" au "Nitawafanya vizazi vyako kuwa taifa kubwa"
# na kulifanya jina lako kuwa kubwa
Neno "jina" linawakilisha sifa ya mtu. "na kukufanya uwe maarufu"
# na utafanyika baraka
neno "jina" linawakilisha sifa ya mtu. "na kukufanya uwe maarufu"
# asiye kuheshimu nita mlaani
"Nitamlaani yeyote atakayekutendea jambo kwa njia ya aibu" au "iwapo kuna mtu atakayekutendea jambo lisilofaa, nitamlaani"
# Kupitia kwako familia zote za nchi zitabarikiwa
Hii inaweza kufanywa katika hali ya kutenda. "Nitabariki familia za nchi kupitia kwako"
# Kupitia kwako
"Kwa sababu yako" au "Kwa sababu nimekubariki"