# Sasa Neno hili linatumika kuweka alama sehemu mpya ya simulizi. # Nenda utoke katika nchi yako, na toka kwa ndugu zako "Nenda kutoka nchini kwako, kutoka katika familia yako" # Nitakufanya uwe taifa kubwa Hapa "nitakufanya" ni umoja na ina maana ya Abramu, lakini Abramu anawakilisha vizazi vyake. "Nitaanzisha taifa kubwa kupitia kwako" au "Nitawafanya vizazi vyako kuwa taifa kubwa" # na kulifanya jina lako kuwa kubwa Neno "jina" linawakilisha sifa ya mtu. "na kukufanya uwe maarufu" # na utafanyika baraka neno "jina" linawakilisha sifa ya mtu. "na kukufanya uwe maarufu" # asiye kuheshimu nita mlaani "Nitamlaani yeyote atakayekutendea jambo kwa njia ya aibu" au "iwapo kuna mtu atakayekutendea jambo lisilofaa, nitamlaani" # Kupitia kwako familia zote za nchi zitabarikiwa Hii inaweza kufanywa katika hali ya kutenda. "Nitabariki familia za nchi kupitia kwako" # Kupitia kwako "Kwa sababu yako" au "Kwa sababu nimekubariki"