sw_tn/ezk/07/23.md

945 B

Maelezo ya Jumla:

Haya ni maneno ya Yahwe kwa Ezekieli kuhusu Israeli.

Tengeneza mnyororo

Minyororo hutumika kushikilia watumwa au wafungwa. Mungu anasema hivi kuonyesha watu ambao watakuwa watumwa au wafungwa.

nchi imejawa na hukumu ya damu

"kila sehemu katika nchi Mungu anawahukumu watu kwa sababu wamewaua watu wengine vikali sana."

mji umejaa udhalimu

"Udhalimu u kila mahali katika mji" au "watu wengi katika mji wanafanya mambo maovu kwa wengine"

na watamiliki nyumba zao

"waovu watazichukua nyumba za Israeli"

nitaleta mwisho kwenye fahari ya uweza

nitawafanya watu wenye nguvu katika Israeli kuacha kujiona fahari"

mahali pao patakatifu patanajisiwa!

Maadui watapanajisi mahali mnapo abudia."

mahali pao patakatifu

mahali ambapo walipoabudia sanamu.

Hofu itakuja

"Watu watakuwa na hofu"

Wataitafuta amani

"Watatumaini tumaini kwa ajili ya amani" au "Watajaribu kufanya amani pamoja na maadui zao"