# Maelezo ya Jumla: Haya ni maneno ya Yahwe kwa Ezekieli kuhusu Israeli. # Tengeneza mnyororo Minyororo hutumika kushikilia watumwa au wafungwa. Mungu anasema hivi kuonyesha watu ambao watakuwa watumwa au wafungwa. # nchi imejawa na hukumu ya damu "kila sehemu katika nchi Mungu anawahukumu watu kwa sababu wamewaua watu wengine vikali sana." # mji umejaa udhalimu "Udhalimu u kila mahali katika mji" au "watu wengi katika mji wanafanya mambo maovu kwa wengine" # na watamiliki nyumba zao "waovu watazichukua nyumba za Israeli" # nitaleta mwisho kwenye fahari ya uweza nitawafanya watu wenye nguvu katika Israeli kuacha kujiona fahari" # mahali pao patakatifu patanajisiwa! Maadui watapanajisi mahali mnapo abudia." # mahali pao patakatifu mahali ambapo walipoabudia sanamu. # Hofu itakuja "Watu watakuwa na hofu" # Wataitafuta amani "Watatumaini tumaini kwa ajili ya amani" au "Watajaribu kufanya amani pamoja na maadui zao"