sw_tn/col/03/01.md

720 B

Sentensi unganishi:

Paulo anawaonya walioamini kwamba kwa kuwa ni wamoja pamoja na Kristo, kuna mambo ambayo waumini hawapaswi kuyafanya

Mungu amewafufua pamoja na Kristo

Kama vile Mungu alivyo mfufua Kristo kutoka kwa wafu, hivyo anawahesabu waumini wa Kolosai kama waliofufuliwa kwenda mbinguni.

mambo yaliyo juu

"mambo ya mbinguni" au "mambo ya kimungu"

kwa kuwa mmekufa

Kama Kristo alivyokufa, hivyo Mungu anawahesabu waumini wa Kolosai kama wamekufa na Kristo.

maisha yenu yamefichwa pamoja na Kristo

Paulo anazungumzia wale watu waishio kana kwamba walikuwa alama ambayo inayoweza kujificha kwenye chombo cha kubebea.

ambaye ni maisha yenu

Kristo ni yule atoaye uzima wa kiroho kwa waamini.