# Sentensi unganishi: Paulo anawaonya walioamini kwamba kwa kuwa ni wamoja pamoja na Kristo, kuna mambo ambayo waumini hawapaswi kuyafanya # Mungu amewafufua pamoja na Kristo Kama vile Mungu alivyo mfufua Kristo kutoka kwa wafu, hivyo anawahesabu waumini wa Kolosai kama waliofufuliwa kwenda mbinguni. # mambo yaliyo juu "mambo ya mbinguni" au "mambo ya kimungu" # kwa kuwa mmekufa Kama Kristo alivyokufa, hivyo Mungu anawahesabu waumini wa Kolosai kama wamekufa na Kristo. # maisha yenu yamefichwa pamoja na Kristo Paulo anazungumzia wale watu waishio kana kwamba walikuwa alama ambayo inayoweza kujificha kwenye chombo cha kubebea. # ambaye ni maisha yenu Kristo ni yule atoaye uzima wa kiroho kwa waamini.