sw_tn/2sa/17/11.md

36 lines
983 B
Markdown

# kwamba Israeli wote wakusanywe pamoja kwako
Askari wote wanatajwa hapa kama "Israeli wote"
# kutoka Dani hadi Beersheba
Kifungu hiki kinamaanisha kutoka mpaka wa kaskazini hadi mpaka wa kusini wa Israeli
# wengi kama mchanga ulioko ufuweni mwa bahari
Hii ni kuzidisha maana pale chembe zote za mchanga zinalinganishwa na idadi ya askari wa Israeli.
# kwamba wewe mwenyewe unakwenda vitani
Kifungu hiki "binafsi" kinamaanisha kwenda wewe mwenyewe na wala siyo kutuma mtu mwingine.
# kuja juu yake
Hii inamaana ya kwenda kwake kwa kusudi la kumshambulia.
# tutamfunika kama umande unavyofunika ardhi
Jeshi la Absalomu linaelezwa kulifunika jeshi la Daudi kama umande unavyoifunika ardhi wakati wa asubuhi.
# umande
mvuke unaoanguka juu ya ardhi kama maji na kuifunika ardhi wakati wa usiku na kuacha ardhi imeloa.
# Hatutaacha hata mmojawao ... akiwa hai
Sentensi hii imetumika kusisitiza kwamba watamwua kila mtu.
# Yeye mwenyewe
Maneno haya yote yanamtaja Daudi.