# kwamba Israeli wote wakusanywe pamoja kwako Askari wote wanatajwa hapa kama "Israeli wote" # kutoka Dani hadi Beersheba Kifungu hiki kinamaanisha kutoka mpaka wa kaskazini hadi mpaka wa kusini wa Israeli # wengi kama mchanga ulioko ufuweni mwa bahari Hii ni kuzidisha maana pale chembe zote za mchanga zinalinganishwa na idadi ya askari wa Israeli. # kwamba wewe mwenyewe unakwenda vitani Kifungu hiki "binafsi" kinamaanisha kwenda wewe mwenyewe na wala siyo kutuma mtu mwingine. # kuja juu yake Hii inamaana ya kwenda kwake kwa kusudi la kumshambulia. # tutamfunika kama umande unavyofunika ardhi Jeshi la Absalomu linaelezwa kulifunika jeshi la Daudi kama umande unavyoifunika ardhi wakati wa asubuhi. # umande mvuke unaoanguka juu ya ardhi kama maji na kuifunika ardhi wakati wa usiku na kuacha ardhi imeloa. # Hatutaacha hata mmojawao ... akiwa hai Sentensi hii imetumika kusisitiza kwamba watamwua kila mtu. # Yeye mwenyewe Maneno haya yote yanamtaja Daudi.