sw_tn/2sa/17/08.md

36 lines
880 B
Markdown

# Wako kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake
Hasira ya askari hapa inalinganiswa na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake.
# dubu
mnyama mkubwa na mkali anayetembea kwa miguu minne na ana makucha na meno makali
# Mtu wa vita
Hii inamaanisha amepigana vita nyingi na anajua kwa kina njia ya vita.
# Tazama
Neno hili limetumika kuvuta makini ya mtu kwa kile kinachofuata
# shimo
tundu refu katika ardhi
# au katika sehemu ningine
Hili ni eneo lingine analoweza kuwa amejificha.
# baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa
Inamaanisha watu wa Daudi watakapokuwa wamewauwa baadhi ya watu wa Absalomu
# mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu
Nomino "machinjo" inamaanisha tukio ambapo watu wengi wameuawa kwa ukatili.
# ambao mioyo yao ni kama mioyo ya simba
Hapa askari wanatajwa kwa "mioyo" yao. Pia, ujasiri wao mkuu unalinganishwa na ule wa simba.