# Wako kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake Hasira ya askari hapa inalinganiswa na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake. # dubu mnyama mkubwa na mkali anayetembea kwa miguu minne na ana makucha na meno makali # Mtu wa vita Hii inamaanisha amepigana vita nyingi na anajua kwa kina njia ya vita. # Tazama Neno hili limetumika kuvuta makini ya mtu kwa kile kinachofuata # shimo tundu refu katika ardhi # au katika sehemu ningine Hili ni eneo lingine analoweza kuwa amejificha. # baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa Inamaanisha watu wa Daudi watakapokuwa wamewauwa baadhi ya watu wa Absalomu # mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu Nomino "machinjo" inamaanisha tukio ambapo watu wengi wameuawa kwa ukatili. # ambao mioyo yao ni kama mioyo ya simba Hapa askari wanatajwa kwa "mioyo" yao. Pia, ujasiri wao mkuu unalinganishwa na ule wa simba.