Chachu ni kiungo kinachosababisha mkate kuwa kubwa kabla ya kuoka. Katika sura hii, Yesu anatumia chachu kama sitiari ya mambo ambayo yanabadili jinsi watu wanavyofikiri, kuzungumza, na kutenda. (See: [[rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor]])
Wakati Yesu aliwaita watu "kizazi cha uzinzi," alikuwa akiwaambia kuwa hawakuwa waaminifu kwa Mungu. (See: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/faithful]] and [[rc://*/tw/dict/bible/kt/peopleofgod]])
Yesu alitumia maswali mengi yauhuishaji kama njia ya kuwafundisha wanafunzi (Marko 8:17-21) na kuwakaripia watu (Marko 8:12). (See: [[rc://*/ta/man/translate/figs-rquestion]])
Kitendawili ni taarifa ya kweli inayoonekana kuelezea kitu kisichowezekana. Yesu anatumia kitambo wakati anasema, "Yeyote anayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata" (Marko 8:35-37).