sw_tn/1ti/01/03.md

36 lines
983 B
Markdown

# Kauli Unganishi
Paulo anamtia moyo Timotheo kukataa matumizi mabaya ya sheria na atumie vizuri mafundisho kutoka kwa Mungu.
# Kama nilivyokusihi wewe
"Kama nilivyokuhimiza wewe," au "Kama nilivyokuomba kwa bidii"
# kaeni Efeso
"nisubirini mimi hapo katika mji wa Efeso"
# mapokeo mengine
mafundisho mengine tofauti na yale tuliyofundisha sisi.
# wala hawatasikiliza kwa makini
"Pia nataka ninyi muwaamuru wasisikilize kwa makini"
# hadithi
zinaweza kuwa ni hadithi kuhusu mababu zao.
# vizazi visivyo na mwisho
Paulo anatumia "isiyo na mwisho" kusisitiza kwamba vizazi ni vingi.
# Hizi husababisha malumbano
"Hizi huwafanya watu kutokubaliana." Watu walijadili kuhusu hadithi na nasaba ambamo hakuna angeweza kujua ukweli wake.
# badala ya kusaidia mpango wa Mungu, ambao ni kwa imani
Maana: 1) badala ya kutusaidia sisi kujua mpango wa Mungu wa kutuokoa, ambao tunajifunza kwa imani 2) badala ya kutusaidia sisi kufanya kazi ya Mungu, ambayo tunaifanya kwa imani