# Kauli Unganishi Paulo anamtia moyo Timotheo kukataa matumizi mabaya ya sheria na atumie vizuri mafundisho kutoka kwa Mungu. # Kama nilivyokusihi wewe "Kama nilivyokuhimiza wewe," au "Kama nilivyokuomba kwa bidii" # kaeni Efeso "nisubirini mimi hapo katika mji wa Efeso" # mapokeo mengine mafundisho mengine tofauti na yale tuliyofundisha sisi. # wala hawatasikiliza kwa makini "Pia nataka ninyi muwaamuru wasisikilize kwa makini" # hadithi zinaweza kuwa ni hadithi kuhusu mababu zao. # vizazi visivyo na mwisho Paulo anatumia "isiyo na mwisho" kusisitiza kwamba vizazi ni vingi. # Hizi husababisha malumbano "Hizi huwafanya watu kutokubaliana." Watu walijadili kuhusu hadithi na nasaba ambamo hakuna angeweza kujua ukweli wake. # badala ya kusaidia mpango wa Mungu, ambao ni kwa imani Maana: 1) badala ya kutusaidia sisi kujua mpango wa Mungu wa kutuokoa, ambao tunajifunza kwa imani 2) badala ya kutusaidia sisi kufanya kazi ya Mungu, ambayo tunaifanya kwa imani