sw_tn/gal/02/intro.md

1.1 KiB

Wagalatia 02 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaendelea kutetea injili ya kweli. Hii ilianza katika Wagalatia 1:11.

Dhana maalum katika sura hii

Uhuru na utumwa

Katika barua hii, Paulo anatofautisha uhuru na utumwa. Mkristo ana uhuru katika Kristo kufanya mambo mengi tofauti. Lakini Mkristo ambaye anajaribu kufuata sheria ya Musa anahitaji kufuata sheria nzima. Paulo anaelezea kwamba kujaribu kufuata sheria ni kama aina ya utumwa. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/lawofmoses)

hangamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Siibatili neema ya Mungu"

Paulo anafundisha kwamba, ikiwa Mkristo anajaribu kufuata sheria ya Musa, haelewi neema ambayo Mungu amemwonyesha. Hii ni kosa la msingi. Lakini Paulo anatumia maneno "Siibatili neema ya Mungu" kama aina ya hali ya mawazo. Shabaha ya neno hili inaweza kuonekana kama, "Ikiwa ungeweza kuokolewa kwa kufuata sheria, basi hiyo ingeweza kupuuza neema ya Mungu." (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/grace]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-hypo]])

<< | >>