sw_tn/gal/03/intro.md

1.5 KiB

Wagalatia 03 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Usawa katika Kristo

Wakristo wote wameungana kwa usawa na Kristo. Wala uzazi, wala jinsia, wala cheo, vyote havijalishi. Wote wako sawa na wenzake. Wote wako sawa machoni pa Mungu.

Mfano muhimu ya matamshi katika sura hii

Maswali ya uhuishaji

Paulo hutumia maswali tofauti mengi ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kuwashawishi Wagalatia juu ya dhambi zao. (See: [[rc:///ta/man/translate/figs-rquestion]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]])

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mwili

Hili ni suala ngumu. "Mwili" inaweza kuwa mfano ya asili yetu ya dhambi. Paulo hafundishi kwamba sehemu ya kimwili ya mwanadamu ni ya dhambi. "Mwili" hutumiwa katika sura hii kutofautisha na yale ambayo ni ya kiroho. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/flesh)

"Wale wa imani ni watoto wa Abrahamu"

Wasomi wamegawanyika juu ya maana ya maneno haya. Baadhi yao wanaamini kama Wakristo wanarithi ahadi ambazo Mungu alimpa Abrahamu, kwa hiyo Wakristo wanachukua nafasi ya wazao wa Israeli. Wengine wanaamini kama Wakristo hufuata Abrahamu kiroho, lakini hawarithi ahadi ambazo Mung alimpa Abrahamu. Kwa kuzingatia mafundisho mengine ya Paulo na muktadha hapa, Labda Paulo anaandika hivi kuhusu Wakristo wa Kiyahudi na wa Mataifa walio na imani sawa na Abrahamu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/spirit]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]])

<< | >>