sw_tn/eph/05/intro.md

1.5 KiB

aefeso 05 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivi kwa maneno ya mstari wa 14.

Dhana maalum katika sura hii

Urithi wa ufalme wa Kristo

Hii ni vigumu kuelewa. Baadhi ya wasomi wanaamini kuwa wale wanaoendelea kufanya mambo haya hawataurithi uzima wa milele. Lakini Mungu anaweza kusamehe dhambi zote zilizotajwa katika aya hii. Kwa hiyo washerati, wasio wasafi, au wenye tamaa wakingali wanaweza kupata uzima wa milele ikiwa wanatubu na kumwamini Yesu. Somo la asili zaidi ni "Hakuna mtu ambaye ni mzinzi au msherati, au mlafi (kwani hii ni sawa na kuabudu sanamu) atakayekuwa kati ya watu wa Mungu ambao Kristo anatawala kama mfalme." (UDB) (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/forgive]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/eternity]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/life]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/inherit]])

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Wanawake, watii waume zenu

Wasomi wamegawanywa juu ya jinsi ya kuelewa kifungu hiki katika mazingira yake ya kihistoria na ya kitamaduni. Baadhi ya wasomi wanaamini kama wanaume na wanawake ni sawa kabisa katika mambo yote. Wasomi wengine wanaamini kama Mungu aliumba wanaume na wanawake kutekeleza majukumu tofauti katika ndoa na kanisa. Watafsiri wanapaswa kuwa makini wasiweke jinsi wanavyoelewa suala hili kuathiri jinsi wanavyotafsiri kifungu hiki.

<< | >>