sw_tn/eph/04/intro.md

1.1 KiB

Waefeso 04 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kuwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hii kwa mstari wa 8, ambayo imenukuliwa kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Vipawa vya kiroho

Vipawa vya kiroho ni uwezo usio wa kawaida ambao Roho Mtakatifu huwapa Wakristo baada ya kumwamini Yesu. Paulo anataja hapa baadhi tu ya vipawa vya kiroho. Wasomi wengine wanaamini kwamba Roho Mtakatifu alitoa vipawa vya kiroho kwa waumini katika kanisa la kwanza pekee. Vipawa hivi vya kiroho vilikuwa msingi kwa kuendeleza kanisa. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/faith)

Umoja

Paulo anaona kuwa ni muhimu sana kwamba kanisa lina umoja. Hii ni mada kuu ya sura hii.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mtu wa kale na mtu mpya

Neno "mtu wa kale" labda linamaanisha hali ya dhambi ambayo mtu huzaliwa. "Mtu mpya" ni asili mpya au maisha mapya ambayo Mungu humpa mtu baada ya kumwamini Kristo.

<< | >>