sw_tn/jos/05/12.md

28 lines
1.4 KiB
Markdown

# Mana
Mana kilikuwa ni chakula cheupe cha nafaka ambacho Mungu aliwapatia Wana wa Israeli ili wale katika kipindi cha miaka 40 walioishi jangwaani baada ya kuwa wametoka Misri.
* Mana ilionekana kama vipande vyeupe vilivyoonekana juu ya nchi kila asubuhi katika umande. Ilikuwa na ladha tamu kama asali.
* Waisraeli walikusanya mana kila siku isipokuwa siku ya Sabato.
* Siku moja kabla ya Sabato Mungu aliwaambia waisraeli kukusanya mana mara mbili ili wasikusanye siku ya kupumzika.
Neno 'mana' lina maana ya ''Hiki ni nini?"
* Katika Biblia neno 'Mana' pia hurejelewa kama "Mkate kutoka mbinguni" na "nafaka kutoka mbinguni."
# Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli.
Istilahi hii "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Lina maana ya "Alishindana na Mungu."
* Uzao wa Yakobo ulikuja ukajulikana kama "Watu wa Israeli," "taifa la Israeli''l au Waisraeli.
* Mungu alifanya Agano na taifa la Israeli. Walikuwa ni watu wake wateule.
* Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mawili. .
# Kanaani, Wakanaani
Kanaani alikuwa ni mtoto wa Hamu, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wana wa Nuhu. Wakanaani walikuwa ni uzao wa Kanaani.
* Neno "Kaanani" au "nchi ya Kanaani" pia inarejelea sehemu ya nchi iliyo katikati ya Mto Yordani na Bahari Kuu (Meditraniani).
* Nchi hii ilikaliwa na Wakanaani, pamoja na baadhi ya makabila mengine.
* Mungu alimwahidi Ibrahimu kumpa nchi ya Kanaani na uzao wake, yaani Waisraeli.