sw_tn/jos/05/12.md

1.4 KiB

Mana

Mana kilikuwa ni chakula cheupe cha nafaka ambacho Mungu aliwapatia Wana wa Israeli ili wale katika kipindi cha miaka 40 walioishi jangwaani baada ya kuwa wametoka Misri.

  • Mana ilionekana kama vipande vyeupe vilivyoonekana juu ya nchi kila asubuhi katika umande. Ilikuwa na ladha tamu kama asali.
  • Waisraeli walikusanya mana kila siku isipokuwa siku ya Sabato.
  • Siku moja kabla ya Sabato Mungu aliwaambia waisraeli kukusanya mana mara mbili ili wasikusanye siku ya kupumzika.

Neno 'mana' lina maana ya ''Hiki ni nini?"

  • Katika Biblia neno 'Mana' pia hurejelewa kama "Mkate kutoka mbinguni" na "nafaka kutoka mbinguni."

Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli.

Istilahi hii "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Lina maana ya "Alishindana na Mungu."

  • Uzao wa Yakobo ulikuja ukajulikana kama "Watu wa Israeli," "taifa la Israeli''l au Waisraeli.
  • Mungu alifanya Agano na taifa la Israeli. Walikuwa ni watu wake wateule.
  • Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mawili. .

Kanaani, Wakanaani

Kanaani alikuwa ni mtoto wa Hamu, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wana wa Nuhu. Wakanaani walikuwa ni uzao wa Kanaani.

  • Neno "Kaanani" au "nchi ya Kanaani" pia inarejelea sehemu ya nchi iliyo katikati ya Mto Yordani na Bahari Kuu (Meditraniani).
  • Nchi hii ilikaliwa na Wakanaani, pamoja na baadhi ya makabila mengine.
  • Mungu alimwahidi Ibrahimu kumpa nchi ya Kanaani na uzao wake, yaani Waisraeli.