# Mana Mana kilikuwa ni chakula cheupe cha nafaka ambacho Mungu aliwapatia Wana wa Israeli ili wale katika kipindi cha miaka 40 walioishi jangwaani baada ya kuwa wametoka Misri. * Mana ilionekana kama vipande vyeupe vilivyoonekana juu ya nchi kila asubuhi katika umande. Ilikuwa na ladha tamu kama asali. * Waisraeli walikusanya mana kila siku isipokuwa siku ya Sabato. * Siku moja kabla ya Sabato Mungu aliwaambia waisraeli kukusanya mana mara mbili ili wasikusanye siku ya kupumzika. Neno 'mana' lina maana ya ''Hiki ni nini?" * Katika Biblia neno 'Mana' pia hurejelewa kama "Mkate kutoka mbinguni" na "nafaka kutoka mbinguni." # Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli. Istilahi hii "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Lina maana ya "Alishindana na Mungu." * Uzao wa Yakobo ulikuja ukajulikana kama "Watu wa Israeli," "taifa la Israeli''l au Waisraeli. * Mungu alifanya Agano na taifa la Israeli. Walikuwa ni watu wake wateule. * Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mawili. . # Kanaani, Wakanaani Kanaani alikuwa ni mtoto wa Hamu, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wana wa Nuhu. Wakanaani walikuwa ni uzao wa Kanaani. * Neno "Kaanani" au "nchi ya Kanaani" pia inarejelea sehemu ya nchi iliyo katikati ya Mto Yordani na Bahari Kuu (Meditraniani). * Nchi hii ilikaliwa na Wakanaani, pamoja na baadhi ya makabila mengine. * Mungu alimwahidi Ibrahimu kumpa nchi ya Kanaani na uzao wake, yaani Waisraeli.