sw_tn/act/17/01.md

41 lines
1.0 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Habari kuhusu Paulo na Sila inaendelea pamoja na Timotheo katika safari yao ya kimisionari. Walifika Thesalonike na Luka hakuwa pamoja nao.
# Taarifa za jumla
Ni habari kuhusu Paulo na Sila pamoja na Wayahudi katika Sinagogi huko Thesolanike
# Sasa
Ni neno linalogawanya habari iliyokuwa ikiendelea kwa kutaja jambo jingine. Luka anaanza kuelezea sehemu mpya ya tukio.
# walipopita
"Kusafiri kupitia"
# miji ya Amfipoli na Apolonia
Hii ni miji ya mwambao huko Makedonia
# walifika mjini
Neno linaloonyesha kuwa walisafiri hadi kufika mjini.
# kama ilivyokuwa kawaida
" kama ilivyokuwa kawaida yake" au "Kama alivyofanya siku zote". Mara kwa mara Paulo alikuwa na ya kuingia kwenye Sinagogi siku ya sabato mahali wayahudi walikusanyuka.
# kwa sabato tatu
"katika kila siku ya sabato kwa majuma matatu".
# alihojiana nao kutoka kwenye maandiko
"alijadiliana na Wayahudi wa Sinagogi" au walijadili na Wayahudi wa Sinagogi"
# alihojiana nao
"aliwapa sababu" au "kuhojiana pamoja nao" au "kuzungumza pamoja nao".