# Sentensi unganishi Habari kuhusu Paulo na Sila inaendelea pamoja na Timotheo katika safari yao ya kimisionari. Walifika Thesalonike na Luka hakuwa pamoja nao. # Taarifa za jumla Ni habari kuhusu Paulo na Sila pamoja na Wayahudi katika Sinagogi huko Thesolanike # Sasa Ni neno linalogawanya habari iliyokuwa ikiendelea kwa kutaja jambo jingine. Luka anaanza kuelezea sehemu mpya ya tukio. # walipopita "Kusafiri kupitia" # miji ya Amfipoli na Apolonia Hii ni miji ya mwambao huko Makedonia # walifika mjini Neno linaloonyesha kuwa walisafiri hadi kufika mjini. # kama ilivyokuwa kawaida " kama ilivyokuwa kawaida yake" au "Kama alivyofanya siku zote". Mara kwa mara Paulo alikuwa na ya kuingia kwenye Sinagogi siku ya sabato mahali wayahudi walikusanyuka. # kwa sabato tatu "katika kila siku ya sabato kwa majuma matatu". # alihojiana nao kutoka kwenye maandiko "alijadiliana na Wayahudi wa Sinagogi" au walijadili na Wayahudi wa Sinagogi" # alihojiana nao "aliwapa sababu" au "kuhojiana pamoja nao" au "kuzungumza pamoja nao".