sw_tn/2th/01/intro.md

928 B

2 Wathesalonike 01 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Mistari 1-2 huanzisha kirasmi barua hii. Barua za kale katika Mashariki ya Karibu zilikuwa na utangulizi wa aina hii.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni kauli ya ukweli ambayo inaonekana kufafanua kitu kisichoezekana. Kitendawili untaokea katika mistari 4-5: "Tunazungumzia uvumilivu wenu na imani yenu katika mateso yenu yote.Tunazungumzia mateso mnayostahimili.Hii ni ishara ya hukumu ya kweli ya Mungu." Watu kila mara hawangefikiria kwamba kumuamini Mungu wakati wa kuteswa ni ishara ya hukumu ya kweli ya Mungu.Lakini katika mistari ya 5-10, Paulo anaelezea jinsi Mungu atawapatia tuzo wale ambao wanamwamini na jinsi atakavyuwahukumu wanaowatesa. (2 Wathesalonike 1:4-5)