sw_tn/2th/front/intro.md

3.4 KiB

Utangulizi wa 2 Wathesalonike

Sehemu 1: Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa kitabu cha 2 Wathesalonike

  1. Salamu na kushukuru (1:1-3)
  2. WaKristo wanaoumia kwa mateso
    • Wanastahili ufalme wa mbinguni na ahadi yake ya msaada kutoka kwa majaribio (1:4-7)
    • Mungu atawahukumu wale wanaowatesa Wakristo (1:8-12)
  3. Kutoelewa kwa waumini wengine kuhusu kuja kwa Kristo kwa mara ya pili
    • Kurudi wa Kristo haujatokea 2:1-2)
    • Maelekezo kuhusu matukio yatakayotangulia kurudi kwake Kristo (2:3-12)
  4. Imani ya Paulo kwamba Mungu atawaokoa Wakristo Wathesalonike
    • Mwito wake "kusimama imara" (2:13-15)
    • Maombi yake kwamba Mungu atawafariji (2:16-17)
  5. Paulo anatoa ombi la kuombewa na waumini Wathesalonike (3:1-5)
  6. Paulo anatoa amri kuhusu waumini wasiofanya kazi (3:6-15)
  7. Kumalizia (3:16-17)

Nani aliandika 2 Wathesalonike?

Paulo aliandika Wathesalonike 2. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika ufalme nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Paulo aliandika barua hii akiwa anaishi katika mji wa Korintho.

Kitabu cha 2 Wathesalonike kinahusu nini?

Paulo aliandika barua hii kwa waumini katika mji wa Thesalonike. Aliwatia moyo waumini hawa kwa sababu walikuwa wanateswa.Aliwaambia kuendelea kuishi kwa njia inayompendeza Mungu. Alitaka kuwafundisha tena kuhusu kurudi kwa Kristo.

Kichwa cha Kitabu hiki kinastahili kutafsiriwa namna gani?

Watafsiri wanaweza amuru kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "2 Wathesalonike" ama " Wathesalonike wa pili." ama wanaweza chagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama, "Barua ya pili kwa kanisa la Thesalonike," ama "Barua ya pili kwa Wakristo wa Thesalonike," (Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Nini maana ya "ujio wa pili wa Yesu"?

Paulo aliandika maswala mengi katika barui hii kuhusu kurudi kwake Yesu Kristo duniani.Yesu akirudi, atawahukumu wanadamu wote. Pia atahukumu viumbe wote. Atasababisha kuwepo kwa amani duniani. Paulo pia alieleza kwamba "mwanaume mhalifu" atakuja kabla ya kurudi kwa Kristo.Mtu huyu atamtii Shetani na kufanya watu wengi kumuasi Mungu.Lakini Yesu atamuangamizi huyu mtu atakaporudi.

Sehemu 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Paulo alimaanisha na maelezo "ndani ya Bwana," na "ndani ya Kristo,' na kadhalika?

Paulo alitaka kuasilisha swala la muungano wa karibu kati ya Kristo na waumini. Tazama utangulizi wa kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu aina hii ya maelezo.

Ni maswala gani makuu ya maandishi ya kitabu cha 2 Wathesalonike?

Katika mistari ifuatayo, matoleo ya kisasa yanatofautiana na matoleo ya kale.ULB ina masomo ya kisasa na huyaweka masomo ya awali kama maelezo ya chini.Iwapo kuna tafsiri ya Bibilia katika eneo jumla, watafsiri wazingatie kutumia masomo yanayopatikana katika hayo matoleo. Kama sivyo, watafsiri wanashauriwa kufuata masomo ya kisasa.

  • "Na yule mtu wa kuasi anatambulishwa" (2:3). ULB na UDB na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi.Matoleo ya awali yanasoma, "na yule mtu wa dhambi anatambulishwa."
  • "Kwa maana Mungu aliwachagua kama matunda ya kwanza ya wokovu" (2:13) ULB, UDB, na matoleo mengine husoma hivi. Matoleo mengine yanasoma, "Kwa vile Mungu aliwachagua "kutoka mwanzo kwa ajili ya wokovu."

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)