sw_tn/2co/12/intro.md

2.4 KiB

2 Wakorintho 12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaendelea kutetea mamlaka yake katika sura hii.

Wakati Paulo alikuwa pamoja na Wakorintho, alijitokeza kuwa mtume kwa matendo yake yenye nguvu. Yeye hakuwahi kuchukua chochote kutoka kwao. Sasa kwa vile anakuja kwa mara ya tatu, bado hatachukua chochote. Anatarajia kwamba atakapowatembelea, hatahitaji kuwa mkali kwao. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/apostle)

Dhana maalum katika sura hii

Maono ya Paulo

Paulo sasa anatetea mamlaka yake kwa kusema juu ya maono mazuri ya mbinguni. Ingawa anazungumza kama mtu wa tatu katika mistari ya 2-5, mstari wa 7 unaonyesha kwamba alikuwa mtu aliyepata maono. Ilikuwa kubwa sana kiasi cha Mungu kumpa ulemavu ili kumfanya awe mnyenyekevu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/heaven)

Mbingu ya tatu

Wasomi wengi wanaamini kuwa mbingu "ya tatu" ndiyo makao ya Mungu. Hii ni kwa sababu Maandiko pia hutumia "mbingu kutaja anga (mbingu ya kwanza) na ulimwengu kutaja mbingu ya pili").

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Maswali ya hekima

Paulo anatumia maswali mengi ya uhuishaji anapojitetea dhidi ya maadui zake ambao walimshtaki: "Kwa nini mlikuwa wa hadhi ya chini zaidi kuliko makanisa yote, isipokuwa kwamba sikuwa mzigo kwenu?" "Je, Tito aliwatoza kitu? Je, hatukutembea kwa njia ile ile? Je, hatukuenda kwa hatua moja?" na "Je, unadhani wakati huu wote tumejitetea kwako?" (See: rc://en/ta/man/translate/figs-rquestion)

Kejeli

Paulo anatumia kejeli, aina ya kinaya, wakati anapowakumbusha jinsi alivyowasaidia bila gharama. Anasema, "Nisamehe kwa makosa haya!" Pia hutumia kinaya ya kawaida wakati anasema: "Lakini, kwa kuwa mimi ni mwangalifu, mimi ndiye niliyekukuta kwa udanganyifu." Anaitumia kuanzisha utetezi wake dhidi ya mashtaka haya kwa kuonyesha jinsi ambavyo haingewezekana kuwa kweli. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-irony)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

"Kitendawili" ni tamko la kweli ambalo linaonekana kuelezea jambo lisilowezekana. Sentensi hii katika mstari wa 5 ni kitendawili "Sitajisifu, ila juu ya udhaifu wangu." Watu wengi hawajisifu kuhusu kuwa dhaifu. Sentensi hii katika mstari wa 10 pia ni kitendawili: "Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu." Katika mstari wa 9, Paulo anaeleza kwa nini maneno haya yote ni ya kweli. (2 Wakorintho 12: 5)

<< | >>