sw_tn/2co/11/intro.md

3.4 KiB

2 Wakorintho 11 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Katika sura hii, Paulo anaendelea kutetea mamlaka yake.

Dhana maalum katika sura hii

Mafundisho ya uwongo

Wakorintho walikuwa haraka kukubali walimu wa uongo. Walifundisha mambo kuhusu Yesu na injili ambayo yalikuwa tofauti na yasiyo ya kweli. Kinyume na walimu wa uongo, Paulo aliwatumikia Wakorintho kwa moyo wake wote. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/goodnews)

Mwanga

Mwanga hutumiwa kawaida katika Agano Jipya kama mfano. Paulo hapa anatumia nuru ili kuonyesha ufunuo wa Mungu na haki yake. Giza linamaanisha dhambi. Dhambi inatafuta kubaki kufichwa kutoka kwa Mungu. (See: rc://en/tw/dict/bible/other/light]], rc://en/tw/dict/bible/kt/righteous and rc://en/tw/dict/bible/other/darkness and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/sin)

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Mifano

Paulo anaanza sura hii kwa mfano iliyopanuliwa. Anajilinganisha na baba wa bibi harusi ambaye anampa bintiye bikira kwa bwana harusi. Tamaduni za harusi hubadilika kulingana na historia ya kitamaduni. Lakini wazo la kumwonyesha mtu kama mtoto mzima na mtakatifu linaonyeshwa wazi katika kifungu hiki. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor]] and rc://en/tw/dict/bible/kt/holy and [[rc://en/ta/man/translate/figs-explicit)

Kinaya

Sura hii imejaa kinaya. Paulo ana matumaini ya kuwaaibisha waumini wa Korintho kwa kinaya chake.

"Nyinyi huvumilia mambo haya kabisa!" Paulo anadhani kwamba hawapaswi kuvumilia jinsi mitume wa uwongo walivyowafanya. Paulo hafikiri kuwa wao ni mitume hata kidogo.

Taarifa hii, "Kwa maana mnavumilia kwa furaha wapumbavu, ninyi wenyewe ni wenye busara!" ina maana kwamba waumini wa Korintho wanadhani kama walikuwa wenye busara sana lakini Paulo hakubaliani nao.

"Nitasema kwa aibu yetu kwamba tulikuwa dhaifu sana kufanya hivyo." Paulo anazungumza kuhusu tabia anayodhani ni mbaya sana ili kuepuka. Anazungumza kana kwamba anafikiri yeye anafanya makosa kwa kutofanya hivyo. Anatumia swali la uhuishaji pia kama kinaya. "Je, nilikosa kwa kujinyenyekeza ili uweze kuinuliwa?" (See: rc://en/ta/man/translate/figs-irony]] and rc://en/tw/dict/bible/kt/apostle and [[rc://en/ta/man/translate/figs-rquestion)

Maswali ya uhuishaji

Kwa kukataa mitume wa uongo wanaodai kuwa wakuu, Paulo anatumia mfululizo wa maswali ya uhuishaji. Kila swali linahusiana na jibu: "Je, wao ni Waebrania? Nami pia. Wao ni Waisraeli? Nami pia. Wao ni wazao wa Abrahamu? Nami pia. Wao ni watumishi wa Mungu? (Nazungumza kama nimepoteza ufahamu wangu.) Mimi ni zaidi."

Pia hutumia mfululizo wa maswali ya uhuishaji ili atambue shida za waumini wake wapya: "Ni nani aliye dhaifu, na mimi si dhaifu? Ni nani aliyemfanya mwingine kupotea katika dhambi, na mimi sisikiye uchungu?"

"Je, wao ni watumishi wa Kristo?"

Maneno haya ni kejeli, aina maalum ya kinaya inayotumiwa kuchokesha au kutusi. Paulo haamini kuwa walimu hawa wa uongo wanamtumikia Kristo kweli, lakini wanajifanya vile.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

"Kitendawili" ni tamko la kweli ambalo linaonekana kuelezea jambo lisilowezekana. Sentensi hii katika mstari wa 30 ni kitendawili: "Ikiwa ni lazima nijisifu, nitajisifu juu ya kile kinachoonyesha udhaifu wangu." Paulo haelezei kwa nini angeweza kujivunia katika udhaifu wake hadi 2 Wakorintho 12:9. (2 Wakorintho 11:30)

<< | >>