sw_tn/1th/05/04.md

1.2 KiB

ninyi, ndugu hampo kwenye giza

Hapa "ndugu" inamaanisha Wakristo wenzake. "Ninyi si wa dunia hii ya uovu, ambayo ni kama kuwa katika giza"

hata ile siku iwajie kama mwizi

Siku ambayo Bwana atakuja haitakuwa ya kushitukisha kama vile mwizi anavyo mshitukisha mtu. "Isiwapate pasipo kujiandaa"

ninyi nyote ni wana wa mchana...siyo wana wa usiku

Hapa "wana wa mchana" inamaanisha wafuasi wa Kiristo. "wana wa usiku" inamaanisha wale wote wengine wanaofuata dunia.

tusilale kama wengine wafanyavyo

Paulo anafananisha kulala na ile hali ya kutokujua kuwa Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu. " tusiwe kama wengine ambao hawajui kuwa Yesu anarudi tena"

tusilale

neno "tu"inarejea kwa waumii wote .

bali tuendelee kukesha na kuwa na kiasi

Walioamini katika Kristo wanatakiwa wawe katika hali ya tahadhari kwa kurudi kwake na kuwa na kuweza kujizuia,

Kwa kuwa wale walalao hufanya hivyo usiku

Kama ilivyo usiku wakati watu wamelala na hawajui nini kinachotokea, ndivyo itakavyokuwa kwa dunia, ambao hawajui kuwa Kiristo atarudi.

wale wanao lewa hulewausiku

Paulo anataja kuwa ni usiku ambapo watu huwa wanalewa, hivyo kama watu hawana ufahamu kuwa Kiristo anarudi hawataishi maisha ya kujizuia