sw_tn/1th/05/04.md

33 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# ninyi, ndugu hampo kwenye giza
Hapa "ndugu" inamaanisha Wakristo wenzake. "Ninyi si wa dunia hii ya uovu, ambayo ni kama kuwa katika giza"
# hata ile siku iwajie kama mwizi
Siku ambayo Bwana atakuja haitakuwa ya kushitukisha kama vile mwizi anavyo mshitukisha mtu. "Isiwapate pasipo kujiandaa"
# ninyi nyote ni wana wa mchana...siyo wana wa usiku
Hapa "wana wa mchana" inamaanisha wafuasi wa Kiristo. "wana wa usiku" inamaanisha wale wote wengine wanaofuata dunia.
# tusilale kama wengine wafanyavyo
Paulo anafananisha kulala na ile hali ya kutokujua kuwa Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu. " tusiwe kama wengine ambao hawajui kuwa Yesu anarudi tena"
# tusilale
neno "tu"inarejea kwa waumii wote .
# bali tuendelee kukesha na kuwa na kiasi
Walioamini katika Kristo wanatakiwa wawe katika hali ya tahadhari kwa kurudi kwake na kuwa na kuweza kujizuia,
# Kwa kuwa wale walalao hufanya hivyo usiku
Kama ilivyo usiku wakati watu wamelala na hawajui nini kinachotokea, ndivyo itakavyokuwa kwa dunia, ambao hawajui kuwa Kiristo atarudi.
# wale wanao lewa hulewausiku
Paulo anataja kuwa ni usiku ambapo watu huwa wanalewa, hivyo kama watu hawana ufahamu kuwa Kiristo anarudi hawataishi maisha ya kujizuia