# ninyi, ndugu hampo kwenye giza Hapa "ndugu" inamaanisha Wakristo wenzake. "Ninyi si wa dunia hii ya uovu, ambayo ni kama kuwa katika giza" # hata ile siku iwajie kama mwizi Siku ambayo Bwana atakuja haitakuwa ya kushitukisha kama vile mwizi anavyo mshitukisha mtu. "Isiwapate pasipo kujiandaa" # ninyi nyote ni wana wa mchana...siyo wana wa usiku Hapa "wana wa mchana" inamaanisha wafuasi wa Kiristo. "wana wa usiku" inamaanisha wale wote wengine wanaofuata dunia. # tusilale kama wengine wafanyavyo Paulo anafananisha kulala na ile hali ya kutokujua kuwa Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu. " tusiwe kama wengine ambao hawajui kuwa Yesu anarudi tena" # tusilale neno "tu"inarejea kwa waumii wote . # bali tuendelee kukesha na kuwa na kiasi Walioamini katika Kristo wanatakiwa wawe katika hali ya tahadhari kwa kurudi kwake na kuwa na kuweza kujizuia, # Kwa kuwa wale walalao hufanya hivyo usiku Kama ilivyo usiku wakati watu wamelala na hawajui nini kinachotokea, ndivyo itakavyokuwa kwa dunia, ambao hawajui kuwa Kiristo atarudi. # wale wanao lewa hulewausiku Paulo anataja kuwa ni usiku ambapo watu huwa wanalewa, hivyo kama watu hawana ufahamu kuwa Kiristo anarudi hawataishi maisha ya kujizuia