sw_tn/1co/10/intro.md

1.5 KiB

1 Wakorintho 10 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura za 8-10 pamoja zinajibu swali: "Je, inakubalika kula nyama ambayo imetolewa dhabihu kwa sanamu?"

Katika sura hii, Paulo anatumia kutoka kuwaonya watu kutotenda dhambi. Kisha, anarudi kujadili nyama inayotolewa kwa sanamu. Anatumia Mlo wa Bwana kama mfano. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/sin)

Dhana maalum katika sura hii

Kutoka

Paulo anatumia uzoefu wa Israeli kutoka Misri na kutembea jangwani kama onyo kwa waumini. Ingawa Waisraeli walimfuata Musa, wote walikufa njiani. Hakuna hata mmoja aliyefikia Nchi ya Ahadi. Wengine waliabudu sanamu, wengine walimjaribu Mungu, na wengine walinung'unika. Paulo anawaonya Wakristo wasitende dhambi. Tunaweza kushinda majaribu kwa sababu Mungu hutoa njia ya kuepuka. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/promisedland)

Kula nyama iliyotolewa dhabihu kwa sanamu

Paulo anazungumzia nyama iliyotolewa kwa sanamu. Wakristo wanaruhusiwa kula, lakini inaweza kuumiza wengine. Kwa hiyo wakati wa kununua nyama au kukula na rafiki, usiulize ikiwa imetolewa kwa sanamu. Lakini ikiwa mtu anakuambia kuwa imetolewa kwa sanamu, usiile kwa ajili ya mtu huyo. Usimkosee mtu yeyote. Jaribu kuwaokoa badala yake. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/save)

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali mengi ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kusisitiza maneno mmbalimbali anapofundisha Wakorintho.(See: rc://en/ta/man/translate/figs-rquestion)

<< | >>