sw_tn/1co/10/01.md

1.2 KiB

sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha Wakorintho mfano wa tabia ambaya( uovu) na ibada ya sanamu wa baba zao wakongwe wa Kiyahudi

baba zetu

Paulo anarejea kwenye wakati wa Musa katika kitabu cha Kutoka wakati Waisraeli walikimbia kupitia bahari ya chumvi wakati majeshi ya Wamisri yakiwafuatilia. Neno "yetu" linamhusu Paulo mwenyewe pamoja na Wakorintho.

walipita katika bahari

Hii bahari inajulikana kwa majina mawili, Bahari ya chumvi na Bahari ya matete.

walipita

"walipita kwa kutembea" au "walisafiri kupitia"

Wote walibatizwa wawe wa Musa katika wingu

"Wote walimfuata na walijidhatiti kwa Musa"

ndani ya wingu

kwa wingu lililowakilisha uwepo wa Mungu na liliwaongoza Waisraeli wakati wa mchana."mwamba" unawakilisha uimara haswa wa Kristo, ambaye alikuwa pamoja nao wakati wote. Wangetegemea ulinzi na faraja yake.

walikunywa kinywaji kile kile cha roho... mwamba wa roho

" walikunywa maji yale yale ambayo Mungu aliyatoa kwenye mwamba kwa muujiza .... mwamba wa rohoni( mwujiza)

mwamba ule ulikuwa ni Kristo

"mwamba" ulikuwa mwamba wa kawaida ulioonekana kwa macho, hata hivi mwamba huo ulikuwa ukiwakilisha nguvu za Kristo zilizofanya kazi ndani yake " alikuwa Kristo aliyefanya kazi kupitia ule mwamba"