sw_tn/sng/07/07.md

882 B

Maelezo ya Jumla

Mpenzi anaelezea nini angependa kufanya kwa yeye anaye mpenda.

Urefu wako ni wa kama mti wa mtende

"Una simama kama mti wa mtende." Mwanamke ni mrefu, kasimama wima, na anavutia kama mti wa mtende.

mti wa mtende

mti mrefu wa wima unao zalisha matunda matamu ya rangi ya brauni yanayo ota kwa makundi

maziwa yako kama vifungu vya matunda

Mbegu katika mti wa mtende vinaota katika vifungu vizuri vinavyo teremka chini ya mti.

Ninataka kuupanda ... matawi yake

Mwanamme anataka kumshika mwanamke.

Maziwa yako nayawe kama vifungu vya mizabibu

Mwanamke anataka kushika maziwa yake yaliyo kaza lakini malaini kama mizabibu iliyo jawa na maji yake.

harufu ya pua yako yawe kama mapera

"harufu inayo toka kwenye pua yako inukie vizuri kama mapera."

mapera

Neno "mapera" la husu ladha ya tunda tamu, lenye rangi ya njano, aina nzuri ya tunda.