sw_tn/rom/02/08.md

1.0 KiB

Sentensi unganishi:

Japokuwa sehemu hii inazungumzia watu waovu wasio na dini, Paulo anajumuisha kuwa wote wasio Wayahudi na Wayahudi ni waovu mbele za Mungu.

Ubinafsi

Kujitafutia, "choyo" au "mtu anayejali kujipa furaha yeye mwenyewe"

Kutokutii ukweli lakini kutii wasio na haki

Mistari hii miwili ina maana sawa. Ya pili inaelezea ya kwanza.

Ghadhabu na hasira kali itakuja

yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza hasira ya Mungu. "Mungu ataonyesha hasira yake kuu"

Dhiki na shida juu ya

Maneno "dhiki" na "shida" yana maana sawa na hapa yansisitiza namna mbavyo adhabu ya Mungu itakavyokuwa mbaya. "Adhabu mbaya ya Mungu itatokea"

Kwa kila nafsi ya mwanadamu

Hapa Paulo ametumia neno "nafsi" kuonyesha kuwa anamaanisha mtu kwa ujumla. "kwa kila mtu"

Amefanya uovu

"ameendelea kufanya mambo maovu"

Kwa Wayahudi kwanza , na pia kwa Wayunani

"Mungu atawahukumu Wayahudi kwanza, na baada ya hapo atawahukumu ambao sio Wayahudi"

Kwanza

Inaweza kuwa na maana 1) "ya kwanza kwa utaratimu na wakati" au 2) "hakika" au "ya muhimu sana"