sw_tn/rom/02/08.md

36 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi unganishi:
Japokuwa sehemu hii inazungumzia watu waovu wasio na dini, Paulo anajumuisha kuwa wote wasio Wayahudi na Wayahudi ni waovu mbele za Mungu.
# Ubinafsi
Kujitafutia, "choyo" au "mtu anayejali kujipa furaha yeye mwenyewe"
# Kutokutii ukweli lakini kutii wasio na haki
Mistari hii miwili ina maana sawa. Ya pili inaelezea ya kwanza.
# Ghadhabu na hasira kali itakuja
yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza hasira ya Mungu. "Mungu ataonyesha hasira yake kuu"
# Dhiki na shida juu ya
Maneno "dhiki" na "shida" yana maana sawa na hapa yansisitiza namna mbavyo adhabu ya Mungu itakavyokuwa mbaya. "Adhabu mbaya ya Mungu itatokea"
# Kwa kila nafsi ya mwanadamu
Hapa Paulo ametumia neno "nafsi" kuonyesha kuwa anamaanisha mtu kwa ujumla. "kwa kila mtu"
# Amefanya uovu
"ameendelea kufanya mambo maovu"
# Kwa Wayahudi kwanza , na pia kwa Wayunani
"Mungu atawahukumu Wayahudi kwanza, na baada ya hapo atawahukumu ambao sio Wayahudi"
# Kwanza
Inaweza kuwa na maana 1) "ya kwanza kwa utaratimu na wakati" au 2) "hakika" au "ya muhimu sana"