# Sentensi unganishi: Japokuwa sehemu hii inazungumzia watu waovu wasio na dini, Paulo anajumuisha kuwa wote wasio Wayahudi na Wayahudi ni waovu mbele za Mungu. # Ubinafsi Kujitafutia, "choyo" au "mtu anayejali kujipa furaha yeye mwenyewe" # Kutokutii ukweli lakini kutii wasio na haki Mistari hii miwili ina maana sawa. Ya pili inaelezea ya kwanza. # Ghadhabu na hasira kali itakuja yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza hasira ya Mungu. "Mungu ataonyesha hasira yake kuu" # Dhiki na shida juu ya Maneno "dhiki" na "shida" yana maana sawa na hapa yansisitiza namna mbavyo adhabu ya Mungu itakavyokuwa mbaya. "Adhabu mbaya ya Mungu itatokea" # Kwa kila nafsi ya mwanadamu Hapa Paulo ametumia neno "nafsi" kuonyesha kuwa anamaanisha mtu kwa ujumla. "kwa kila mtu" # Amefanya uovu "ameendelea kufanya mambo maovu" # Kwa Wayahudi kwanza , na pia kwa Wayunani "Mungu atawahukumu Wayahudi kwanza, na baada ya hapo atawahukumu ambao sio Wayahudi" # Kwanza Inaweza kuwa na maana 1) "ya kwanza kwa utaratimu na wakati" au 2) "hakika" au "ya muhimu sana"