sw_tn/rev/17/intro.md

1.6 KiB

Ufunuo 17 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii ni uendelezo wa sura iliyopita.

Dhana muhimu katika sura hii

Kahaba

Wayahudi walionyeshwa mara nyingi kama watu wazinzi na wakati mwingine kama mkahaba. Hayo siyo maelezo yalioko hapa. Muktadha huu unamtambulisha shetani kama kahaba lakini mtafsiri ayafanye haya maelezo yasiwe wazi kabisa. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/writing-apocalypticwriting)

Vilima saba

Huenda hii inaashiria mji wa Roma uliosemekana kujengwa juu ya vilima saba. Hata hivyo, mtafsiri asijaribu kutambulisha hivi vilima saba katika tafsiri.

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

Mifano

Yohana anatumia mifano nyingi katika sura hii. Anapeyana maelezo fulani ya maana yazo lakini anaziacha kubaki kutoeleweka kwa kiwango fulani. Mtafsiri ajaribu kufanya namna hivyo. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Na yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kuja "

Kauli hii imekusudiwa kutoa utofautisho na kauli ya kwamba Yesu "alikuwa na yuko na yu tayari kuja" ambayo imetumika kwingine kwenye maandiko (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-explicit)

Matumizi ya ukweli kinza

Ukweli kinza ni kauli ambayo inaonekana kujipinga ingawa siyo ya kipumbafu. Sentenzi katika 17:11 ni ukweli kinza"yule mnyama ...ni mfalme wa nane ingawa pia ni mmoja wa wale wafalme saba." Mtafsiri asijali kutatua ukweli huu kinza na ubakie kuwa siri. (Ufunuo 17:11)

<< | >>