sw_tn/rev/17/01.md

24 lines
675 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Yohana anaanza kueleza sehemu ya maono yake kuhusu kahaba mkuu.
# hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi
Nomino "hukumu" linaweza kuelezwa na kitenzi "kuhukumu". "jinsi gani Mungu atamhukumu kahaba mkuu aliyeketi juu ya maji mengi"
# kahaba mkuu
"kahaba ambaye kila mmoja anamfahamu." Anawakilisha mji flani wenye uovu.
# juu ya maji mengi
"juu ya mito mingi"
# na juu ya mvinyo wa uasherati wake wakaao duniani wameleweshwa
Divai inawakilisha uasherati. "Watu wa duniani walilewa kwa kunywa divai yake, ambayo ni, walikuwa washerati"
# uasherati wake
Hii inaweza kuwa na maana mbili: uasherati miongoni mwa watu na pia kuabudu miungu.