# Taarifa ya Jumla: Yohana anaanza kueleza sehemu ya maono yake kuhusu kahaba mkuu. # hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi Nomino "hukumu" linaweza kuelezwa na kitenzi "kuhukumu". "jinsi gani Mungu atamhukumu kahaba mkuu aliyeketi juu ya maji mengi" # kahaba mkuu "kahaba ambaye kila mmoja anamfahamu." Anawakilisha mji flani wenye uovu. # juu ya maji mengi "juu ya mito mingi" # na juu ya mvinyo wa uasherati wake wakaao duniani wameleweshwa Divai inawakilisha uasherati. "Watu wa duniani walilewa kwa kunywa divai yake, ambayo ni, walikuwa washerati" # uasherati wake Hii inaweza kuwa na maana mbili: uasherati miongoni mwa watu na pia kuabudu miungu.