sw_tn/rev/11/10.md

36 lines
1013 B
Markdown

# watafurahi kwa ajili yao na kusherekea
"watafurahi kwamba mashahidi wawili wamekufa"
# hata kutumiana zawadi
Hili tendo linaonesha jinsi gani watu walivyofurahi.
# kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nch
Hii ndio sababu watu walifurahi sana kwamba mashahidi wamekufa.
# siku tatu na nusu
"Siku 3 kamili na nusu moja ya siku" au "siku 3.5" au "siku 3 1/2"
# pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia
Uwezo wa pumzi unazungumziwa kama kitu kinachoweza kuingia ndani ya watu. "Mungu atasababisha mashahidi wawili kupumua tena na kuishi"
# Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona
Hofu inazungumziwa kama kitu kinachoweza kuwaangukia watu. "Wale watakao waona wataogopa sana"
# Kisha watasikia
Maana zinazowezekana ni 1) mashahidi wawili watasikia au 2) watu watasikia kile wanachoambiwa mashahidi wawili.
# sauti kuu kutoka mbinguni
Neno "sauti" inammanisha ni yule anayenena. "mtu anazungumza nao kwa sauti kuu toka mbinguni na"
# ikiwaambia
"ikiwaambia mashahidi wawili"