# watafurahi kwa ajili yao na kusherekea "watafurahi kwamba mashahidi wawili wamekufa" # hata kutumiana zawadi Hili tendo linaonesha jinsi gani watu walivyofurahi. # kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nch Hii ndio sababu watu walifurahi sana kwamba mashahidi wamekufa. # siku tatu na nusu "Siku 3 kamili na nusu moja ya siku" au "siku 3.5" au "siku 3 1/2" # pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia Uwezo wa pumzi unazungumziwa kama kitu kinachoweza kuingia ndani ya watu. "Mungu atasababisha mashahidi wawili kupumua tena na kuishi" # Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona Hofu inazungumziwa kama kitu kinachoweza kuwaangukia watu. "Wale watakao waona wataogopa sana" # Kisha watasikia Maana zinazowezekana ni 1) mashahidi wawili watasikia au 2) watu watasikia kile wanachoambiwa mashahidi wawili. # sauti kuu kutoka mbinguni Neno "sauti" inammanisha ni yule anayenena. "mtu anazungumza nao kwa sauti kuu toka mbinguni na" # ikiwaambia "ikiwaambia mashahidi wawili"