sw_tn/psa/132/015.md

16 lines
557 B
Markdown

# Kauli Unganishi:
Mungu anaendelea kuzungumzia mji wa Sayuni kana kwamba Sayuni ni mwanamke.
# Nitambariki sana
"Nitambariki sana Sayuni"
# Nitawaridhisha maskini wake kwa mkate
Hapa "maskini" inamaanisha watu maskini waliomo Sayuni. Hapa "mkate" inaweza kumaanisha chakula kwa ujumla. "Nitawaridhisha watu wa Sayuni kwa chakula"
# Nitawavika makuhani wake na wokovu
Wokovu unazungumziwa kana kwamba ni nguo. Maana zinazowezekana ni 1) "Nitawasababisha makuhani kuenenda kwa namna inayostahili ya wale niliowaokoa" au 2) "Nitawaokoa makuhani wake"