# Kauli Unganishi: Mungu anaendelea kuzungumzia mji wa Sayuni kana kwamba Sayuni ni mwanamke. # Nitambariki sana "Nitambariki sana Sayuni" # Nitawaridhisha maskini wake kwa mkate Hapa "maskini" inamaanisha watu maskini waliomo Sayuni. Hapa "mkate" inaweza kumaanisha chakula kwa ujumla. "Nitawaridhisha watu wa Sayuni kwa chakula" # Nitawavika makuhani wake na wokovu Wokovu unazungumziwa kana kwamba ni nguo. Maana zinazowezekana ni 1) "Nitawasababisha makuhani kuenenda kwa namna inayostahili ya wale niliowaokoa" au 2) "Nitawaokoa makuhani wake"