sw_tn/psa/099/001.md

32 lines
931 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# mataifa
Hii inamaanisha watu wa mataifa. "watu wa mataifa yote"
# yatetemeke
kutetemeka kwa hofu
# Ameketi amesimikwa juu ya makerubi
Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba kiti cha enzi ambacho yahwe hukaa ni juu ya makerubi kwenye mfuniko wa amri za sanduku la agano hekaluni.
# inatetemeka
inatikisika
# Yahwe ni mkuu Sayuni; ameinuliwa juu ya mataifa yote
"Sio tu kwamba Yahwe ni mkuu sayuni, ametukuka juu ya mataifa yote" au "Sio tu kwamba Yahwe anatawala Sayuni, anatawala juu ya mataifa yote"
# ameinuliwa juu ya mataifa yote
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu katika mataifa yote wanamtukuza" au "watu katika mataifa yote wanamsifu sana"
# Acha walisifu jina lako kuu na la ajabu
Hapa mwandishi anahama kutoka kumzungumzia Mungu na kuzungumza na Mungu. Ingawa baada ya msemo huu, anarudi tena kumzungumzia Mungu.